Jumanne , 4th Aug , 2015

Muungano wa makampuni katika utendaji kazi katika biashara imetajwa kuwa ni moja wapo ya changamoto zinazosababisha kudhoofisha uzalishaji wa bidhaa na kufa kwa viwanda vingi katika nchi ya Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika Mkuu wa idara ya makubaliano ya ushindani wa kibiashara katika tume ya ushindani FCC Shedraki Nkelebe katika warsha ya siku mbili yenye lengo la kujadili utafiti ulifanywa na taasisi ya REPOA

Utafiti huo ni kuhusiana na kuongeza kasi ya utekelezaji wa sera na sheria ya ushindani ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki amesema muunganiko huo husababisha kukosekana kwa bidhaa muhimu na kuongezeka kwa athari ambazo hazimlindi mlaji.

Aidha Nkelebe ametoa wito kwa wajasiriamali wadogo kutokuogopa kuingia katika ushindani na kampuni za uzalishaji za ndani nna nje ya nchi kwa kuungana katka vikundi ili waweze kupata mitaji mikubwa kutoka taassi za fedha ili kuwasadia katika kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake mtafiti na mchambuzi wa sera kutoka Repoa Bw. Stephen Wandera amesema Kutokana na utafiti waliofanya umeonesha ni nchi mbili tu ambazo ni Tanzania na Kenya ambazo zimefanikiwa katika utekelezaji wa sera hiyo paoja na kuwepo na mapungufu katika utekelezaji wake katika sekta binafsi na sekta nyingine.

Ameongeza Katika warsha hiyo ambayo lengo kubwa ni kuangalia ushindani unakuwepo bila matatizo yoyote kwa kuangalia jinsi ya kumnufaisha mtumiaji wa kawaida.