Waislam wakiwa katika swala (Picha na Maktaba).
Katika hotuba zilizosomwa na viongozi hao katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida ambapo walifanyia ibada ya swala Iddi viongozi hao wamesema vitendo vinavyofanywa na jamii kwa sasa havikubaliki katika jamii yoyote.
Akizungumza katika viwanja vya Ukombozi ambapo swala ya Idd el Fitri iliswalishwa na Sheikh Issa Nassoro, amesema nchi kwa kukosa uadilifu inaweza kuingia katika machafuko hivyo jamii haina budi kufanya uadilifu katika maeneo yao ya kujitafutia riziki.
Aidha, akaitaka jamii ya waislam kuwa makini na baadhi ya wanasiasa ambao wengi wao baada ya kumalizika kwa bunge wameingia mtaani kwa ajili ya kusambaza chuki juu ya wao wenyewe kwa wenyewe jambo ambalo linaweza kuhatarisha amani ya nchi.
Na katika viwanja vya Mitunduruni Mkoani humo Sheikh wa Wilaya ya Singida Issa Ramadhani ameonyesha kukerwa na watu wanaofanya mauaji kwa kutumia dini ya Kiislam.




