Alhamisi , 7th Aug , 2014

Idara ya uhamiaji mkoani Kigoma, imewakamata raia 26  wa Burundi na wawili kutoka kongo DRC na Rwanda, baada ya kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria .

Baadhi ya wahamiaji haramu waliokamatwa Kigoma

Idara ya uhamiaji mkoani Kigoma, imewakamata raia 26  wa Burundi na wawili kutoka kongo DRC na Rwanda, baada ya kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria .

Idara hiyo pia imewarejesha raia 11 wa burundi waliomaliza kifungo baada ya kuhukumiwa mwaka mmoja uliopita kwa makosa ya kuingia nchini bila vibali.

Afisa uhamiaji mkoa wa kigoma Ambrose Mwanguku amesema raia hao ambao wamekuwa wakitumia njia zisizo rasmi kuingia nchini wamekamatwa mjini kigoma pamoja na katika kijiji cha kalinzi, kufuatia oparesheni inayoendeshwa na maafisa uhamiaji, ambapo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola, ili kufanikisha kampeni ya kuhakikisha watu wote wanaoishi nchini kinyume cha sheria wanaondoka.

Kwa upande wao baadhi ya raia wa Burundi waliokamatwa wamesema wengi wa vijana wa Burundi wanaoingia nchini wanakuja kwa lengo la kufanya kazi za shamba kutokana na hali ngumu ya ajira nchini mwao, huku wengine wakiwa wameoana na watanzania