Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imewakamata wahamiaji haramu wapatao 553 nchini Tanzania katika operesheni ilioyofanyika kati ya tarehe 8 Januari mpaka tarehe 15 Januari mwaka huu, katika mikoa yote hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji (DCIS) Bw. Abbas Irovya wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu operesheni inayoendelea ya kuwabaini watu wanaoishi nchini kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Kwa mujibu wa Bw. Irovya wahamiaji kutoka nchi ya China wanaongoza kwa kuwa na wahamiaji haramu 261, wakifuatiwa na Burundi wakiwa na wahamiaji 138 na tayari baadhi yao wamehojiwa na kuruhusiwa na wengine kurejeshwa nchini mwao na wengine kupelekwa kwenye kambi za wakimbizi za hapa nchini.
Aidha, Bw. Irovya amewataka Watanzania kuendelea kushirikiana na Idara ya Uhamiaji kutoa ripoti mbalimbali za wahamiaji waliopo nchini kinyume cha sheria ili wafuatiliwe..



