Ijumaa , 18th Nov , 2016

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Tate Ole-Nasha amewatakata wafugaji nchini kufuga kibiashara na kuachana na tabia ya kufuga kama desturi.

William Ole Nasha

 

Mhe. Ole Nasha ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na EATV ilipotaka kujua serikali imefanya jitihada gani katika kuweka mazingira wezeshi kwa wafugaji ili waweze kufuga na kuzalisha kwa tija.

Amesema katika kuhakikisha mifugo inachangia katika kukuza pato la taifa na mtu mmoja mmoja serikali tayari imeanza kuwafundisha wafugaji kufuga kibiashara na kuwaboreshea miundombinu bora.

Kwa upande wa ujenzi wa viwanda vya nyama amesema tayari wameanza ujenzi wa kujenga viwanda vya kuchakata nyama nchini.