Jumatatu , 23rd Mei , 2016

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2016, George Mbijima, amewataka wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji kulipa kodi za serikali ili kuongeza pato la taifa.

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2016, George Mbijima.

Akizungumza wakati Mwenge wa Uhuru ulipoweka jiwe la msingi katika mradi wa bandari kavu iliyopo kijii cha Kazimzumbwi wilayani Kisarawe, Mbijima aliwataka wafanyabishara kuwa marafiki na serikali kwa kulipa kodi zinatakiwa bila kukwepa.

Mbijima amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea kodi na ushuru mbalimbali, hivyo endapo wawekezaji na wafayabiashara wakubwa na wadogo wakikaidi ama kutumia njia za panya watakosesha mapato taifa.

Aidha, Kiongozi wa mbio za Mwenge amewaasa wawekezaji hao nchini kujenga tabia ya kushiriki na kuchangia katika miradi mbalimbali ya kijamii pasipo kugomea kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria na taratibu za nchi.