Jumanne , 19th Mei , 2015

Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi amewataka Wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kuwekeza nchini Msumbiji kwa kuwa nchi hiyo ina fursa nyingi ambazo zinahitaji wawekezaji kutoka nje.

Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi.

Nyusi amesema hayo kazika Ziara yake iliyomutanisha na wafanyabiashara nchini na kuongeza kuwa serikali yake imeendelea kujipanga kuhakikisha inafungua milango zaidi kwa wafanyabiashara wa nje kwenda kuwekeza nchini humo na kuongeza kuwa serikali hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kukuza suala la kukuza uchumi ni muhimu kwa maendeleo ya msumbiji.

Kwa upande wake Waziri wa nchi Uwekezaji na Uwezeshaji, nchini Tanzania Christopher Chizza amesema kuwa serikali itaendelea kutoka ushirikiano kwa wale watakaojitokeza kuwekza nchini humo.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya sketa binafsi TPSF, Godfrey Simbeye amesema ziara ya rais huyo imekua na faida kubwa kwa familia ya Wafanyabiashara nchini Tanzania na kusema huo ndio mwanzo mzuri wa Watanzania kwenda kuweka nchini humo.