Jumamosi , 26th Nov , 2016

Wamilki wa leseni za uchimaji mdogo wa madini wa Joshua Mine na Sekeknke one mine wa Sekenke Mkoani Singida, wametozwa faini ya shilingi milioni 10 kila moja kwa kosa la uchafuzi wa mazingira wa kutumia vibaya madini ya zebaki.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akinyooshea kidole sehemu inayoonekana kuwa na maji katika Ziwa Kitangiri Wilayani Iramba.

 

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeitoza faini hiyo kupitia mratibu wa wa Baraza la Kanda a Ziwa Bw. Jamali Baruti na kiwataka wamiliki hao kulipa faini hiyo ndani ya siku 14.

Adhabu hiyo inatokana na makelele katika eneo la uchimbaji, kusambaa kwa vumbi lisilovumilika, kukosekana kwa vyoo pia na matumizi mabaya ya miti katika uchimbaji wao ambao huenda sambamba na uharifu wa misitu.

Sehemu ya viongozi wa Mkoa wa Singida Pamoja na wadau , Wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (hayupo Pichani) katika kikao cha pamoja cha kupokea ripoti ya Mazingira ya Mkoa

 

Aidha baraza limewataka wachimbaji hao kuwa na vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira pamoja na leseni ya uchimbaji.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wiaya ya Mkalama Mhandisi Joakim Masakala  akimuwakilisha mkuu wa wiaya ya Iramba, alisema kuwa ni vizuri wakazi wa maeneo hayo wanavyojibidiisha katika kazi lakini ni muhimu sana kuzingatia afya kwani uchimbaji wa kutumia madini aina ya zebaki bila vifaa salama kazini unaweza kuleta maradhi hususan ya saratani kwani madini hayo hupenya kirahisi katika mwili wa binadamu.

Katikati   Bwana Jamal Baruti Mratibu wa Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira NEMC kanda ya ziwa,  akitoa adhabu kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini, pembeni yake ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Bwana Baruti.

 

Awali katika kikao na uongozi wa mkoa pamoja na wadau wa mazingira Naibu Waziri Luhaga Mpina alitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya mazingira ikiwemo matumizi ya mifuko ya plastic na kuwashauri wakazi wa Singida kutunza mazingira akitolea mfano wa ziwa Kitangiri lililo hatarini kutoweka kabisa.