Alhamisi , 30th Jun , 2016

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewasimamisha kuhudhuria vikao kwa muda vipindi tofauti wabunge watatu wa Chadema, kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu pamoja na kusema uongo bungeni.

Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi

Waliosimamisha kuhuduria vikao ni Mhe. Joseph Mbilinyi kwa kipindi cha vikao 10 kwa kosa kutoa ishara ya tusi bungeni, Mhe. Saed Kubenea na Mhe. James Ole Malya ambao wote wamesimamisha vikao vitano kwa kusema uongo bungeni.

Akizungumza bungeni leo Mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge, Mhe. George Mkuchika, amesema kuwa kamati imejiridhisha kutoka na uchunguzi na ushahidi walioupata juu ya Mhe. Mbilinyi kuonyesha ishara ya matusi wakati akiwa anatoka bungeni.

Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Ackson Tulia, aliwafungia Mhe. Saed Kubenea akituhumiwa kusema uongo dhidi ya Waziri wa Ulinzi na JKT, Mhe. Hussein Mwinyi huku Mhe. Ole Millya akituhumiwa kusema uongo dhidi ya Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama.

Mhe. Tulia amesema maamuzi ya adhabu hiyo imeendelea kuwa kama alivyoitoa kutokana na wabunge hao kutokuwepo bungeni hapo hivyo kukosa nafasi ya kujitetea ili kupunguziwa adhabu aliyoitoa.