Jumanne , 18th Aug , 2015

WANAHABARI nchini wametakiwa kuwa mabalozi wa uandishi wa habari za mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuiokoa dunia na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayo tokea kwa kasi.

Mkurugenzi wa Huduma za Utafiti na Matumizi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa ufafanuzi kwenye warsha ya wadau kuhusu hali ya Hewa

Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya hali ya hewa wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Dr. Ladislaus Chang’a wakati wa kutoa elimu kwa baadhi ya wakulima, wapima mvua na waandishi wa habari Mkoani Njombe.

Amesema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuhakikisha kila mara wanawakumbusha wananchi kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na madhara yake.

Amesema kuwa katika kipindi hiki waandishi wasipo wakumbusha wananchi mara kwa mara juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi mazingira yataendelea kuharibika, na joto kuongezeka maradufu.

Aidha nao waandishi wamelalamikiwa kubandwa na wamiliki wa vyombo vya habari kwa kupewa mda mchache kwa mambo ya kutoa elimu kwa uma huku wakitoa ushauri kwa mamlaka kubadilisha mfumo wa utoaji wa taarifa za utabili wa hali ya hewa.

Raymond Francis Mwandishi, amesema kuwa mamlaka inatakiwa kubadilisha mfumo wa kutoa taarifa hizo kwa kuzilainisha ili kupata watu wanao zifuatilia kwa wingi kuliko zinavyo tolewa na muda wa kutoa taarifa hizo.