Jumatatu , 12th Jun , 2023

Takriban watu 13,000 wamehamishwa kaskazini mashariki mwa Ufilipino wakati volkano maarufu zaidi nchini humo, Mayon, ikiendelea kuvuma kwa kasi.

Malori na magari ya kubeba mizigo yamebeba watu wanaoishi ndani ya eneo la hatari la kudumu au eneo la kilomita sita walikimbilia kwenye makazi.

 Volkano hiyo ya  Mayon ilianza kusugua lava wiki iliyopita. Lakini uhamishaji watu ulianza tu mwishoni mwa wiki wakati shughuli za volkano zilipoongezeka, kuweka tahadhari.Watu zaidi

Volkano hiyo imekua na utulivu katika wiki za hivi karibuni na matetemeko ya mara kwa mara na miamba kuanguka kutoka kwa crater yake.Kitengo cha Volkano nchini humo kinasema Kuna hatari ya mkondo wa haraka wa gesi za volkano na miamba kutoka kwenye crater na kwamba hali hiyo inaleta ugumu.  

Historia inaonyesha kwamba Mlipuko wa mwaka 1814 nchini Ufilipino  uliua watu 1,200 na kuuzika mji mzima.  Lakini pia volcano ya  Mayon ambayo inatoa mwangaza wa  rangi nyekundu, watalii pia wameanza kupiga kambi katika vilima ili kushuhudia tamasha la volkano. Mayon, ambayo Guinness inaielezea kama volkano "ya kawaida zaidi" duniani, ni kivutio cha utalii.