Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB ) imesema kuwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoonekana kushika kasi hivi sasa imewalazimu kutumia njia za mitandao ya kijamii katika kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo nchini Tanzania.

Akiongea na East Africa Radio Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB Bw Geofrey Tengeneza amesema kuwa kupitia mitandao ya kijamii wamefungua portal maalum na nyenzo itakayowezesha watalii kupata taarifa muhimu zinazohusu malazi, usafiri na 'booking' za hoteli na vivutio ambavyo wanataka kutembelea hata kabla hawajafika nchini.

Aidha, Tengeneza amesema kwa kutumia nyenzo maalum watalii wataweza kulipia gharama za kutalii moja kwa moja kwa sehemu husika bila ya kupitia kwa madalali hali mabayo itadhibiti uvujaji wa mapato.