Viongozi sita wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) wamekamatwa na Polisi mjini Dodoma kwa madai ya kukusudia kuikashifu Serikali.
Katika siku za karibuni, viongozi wa Bavicha wamekuwa wakitoa matamko mbalimbali ya kuwahamasisha wafuasi wake kwenda Dodoma kwa kile walichoeleza kuwa ni kuisaidia polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM uliopangwa kufanyika Julai 23 kwa madai kuwa jeshi hilo lilishapiga marufuku mikutano ya kisiasa.
Awali polisi waliwakamata Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, Julius Mwita, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya, George Tito, Katibu Mwenezi wa Bavicha, Edward Simbeye na Katibu Bavicha Wilaya ya Temeke, Hilda Newton, na baadaye Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema, Joseph Kasambala aliyekamatwa baada ya kwenda kituo cha polisi kwa lengo la kuwawekea dhamana wenzake.


