Wameyasema hayo mbele ya mkuu wa wilaya hiyo huku wakiongeza kuwa licha ya kupinga zoezi hilo lisifanyike viongozi walichukua maamuzi ya kuuza maeneo hayo bila kuwashirikisha wanakijiji.
"Hawataki kuheshimu maamuzi ya wananchi tulisema kwamba mali ya kijiji iheshimiwe kuna mali zinauzwa kijanja kijanja lakini tulisema ile mali iheshimiwe na asijenge mtu maana mali ya kijiji wakianza kujenga italeta migogoro badae makesi(kesi) kwa mbele mtu unampa ajenge .....kwa mfano mali gani ...kiwanja cha kijiji kimejengwa na raia sasa huyo raia aliyejenga akisema kwamba nimejenga kwa milioni 100 mnirudishie nani atarudisha? viongozi ndio wanafanya makosa ya kuuza viwanja kwa ujanja ujanja mwenyekiti tulimkataza kwamba hicho kiwanja kisimame kisijengwe lakini sasa hivi kimejengwa kimepauliwa kimepigwa na lipu"MASAKA MIFUKO,Mkazi wa Ngulyati.
"Kuna maeneo ya kijiji yanauzwa kinyemela mengine yanagawiwa kinyemela bila kufuata utaratibu juzi tulikataa kwamba maeneo yale wayaache kama yalivyo tukakataa kwenye mkutano mkuu wa kijiji lakini tukashangaa ujenzi unaendelea" EMMANUEL FARU,Mkazi wa Ngulyati.
Akijibu tuhuma hizo mwenyekiti wa kijiji hicho Lenard Oscar amesema yeye ana miezi minne tangu aingie madarakani kutokana na mtangulizi wake kufariki na eneo hilo kulikuwa na jengo lenye kibanda kimoja cha duka
"Eneo hilo limekwenda limekwenda limefika kwenye hatua za mwishoni mwishoni basi mwenzangu aliyekuwepo akatangulia mbele za haki kitu cha kwanza ilikuwa ni kuwaitisha wananchi mkutano waje walishindwa kuendelea wakasema jamani ee tunaomba maeneo hayo yote ya kijiji yasiendelee na ujenzi wowote ule kilichofanyika kwasababu mwananchi yule alikuwa hajanunua pale na alikuwa hajatoa chochote pale nilimuita mhe,diwani,nilimuita mtendaji wa kata tukakalishana chini tukazungumza mtu huyu kwakweli hakutoa hata mia lakini yupo anajenga pale kwa nia njema ingawaje hazikufuatwa sheria kilichozungumzwa na viongozi na kutoa ushauri ni kwamba ebu kwa kuwa amemaliza ujenzi ule tumuite tumhoji tujue labda alitoa rushwa sehemu yoyote walimuita akasema sikutoa rushwa yoyote ile basi tukampa mtendaji wa kata jukumu amtafute mwanasheria wa halmashauri kwaajili ya kumfungisha mkataba mtu yule kwamba sasa bwana utakuwepo hapa kwa utaratibu moja mbili tatu utakuwa mpangaji kwa siku hizi hapa kwa gharama ambazo umegharamika pale..."kabla hamjafikia hatua hiyo mlirudi kwa wananchi kuwaambia"....hapana hatukurudi tena kwao labda penginepo haya ambayo unayasema ndio makosa mengine ambayo yanajitokeza badae unashindwa kwenda vizuri na wananchi hawa"LENARD OSCAR,Mwenyekiti wa kijiji cha Ngulyati
Mkuu wa wilaya ya Bariadi akawataka viongozi kuheshimu maamuzi ya wananchi.
"Ni vizuri tuwaheshimu wananchi tusifanye maamuzi yoyote bila kuwashirikisha wananchi tukisema tunawapuuza hawa tunafanya maamuzi na kuamini kwamba hawajui tutakuwa hatuwatendei haki kwahiyo nasisitiza umuhimu wakuwaheshimu wananchi na kutii kwasababu mamlaka mliyonayo inatokana na wao"SIMON SIMALENGA,Mkuu wa wilaya ya Bariadi.