Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe,
Hayo yamezungumzwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe alipokuwa anazungumza na vijana katika uzinduzi wa mafunzo ya ujasiriamali chini ya mpango wa “Kijana Jiajiri.”
Mpango huo wa kijana jiajiri unawalenga vijana kati ya miaka 18 hadi 35 unatekelezwa na taasisi ya kuendeleza ujasirimali na ushindani Tanzania (TECC), kwa kushirikiana na taasisi ya kuendeleza vijana kibiashara ya Uingereza (YBI), na baraza la taifa la Uwezeshaji (NEEC).
Dkt. Rutengwe amesema kuwa vijana wengi wanaingia katika biashara bila ya uelewa mpana wa biashara na kutambua namna ya kukabiliana na ushindani wa masoko.
Aidha mkuu huyo wa mkoa ameiomba TECC kutoishia katika manispaa ya Morogoro na badala yake waende katika manispaa nyingine ili kuwajengea uwezo vijana wengine katika ufanyaji biashara.