Mbunge wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Neema Mgaya
Hayo yameelezwa jana jijini Dar es salaam na Mbunge wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Neema Mgaya wakati akiongea na East Africa Radio na kuongeza kuwa vijana ni zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu nchini na kuwataka kutumia fursa zilizopo ikiwemo ya uchaguzi wa serikali za mtaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kuleta mabadiliko katika jamii.
Mh. Mgaya amesema vijana wengi wamekuwa hawaaminiki katika uongozi kutokana na kutokupata mafunzo ya uongozi Pia amewataka vijana kuachana na utegemezi na tabia ya ubinafsi, badala yake wajiunge na vikundi ili waweze kuleta fursa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali nchini.
Bi. Neema ameongeza kuwa vijana wengi wanajiweka nyuma hasa ikifika wakati wa uchaguzi iwe kwenywe kupiga kura au kupigiwa kura huku wakiwa wanahitaji mabadiliko na hawajui kama mabadiliko yanatakiwa kuanza kwao wenyewe.