Jumanne , 21st Apr , 2020

Mchungaji wa Kanisa la KKKT Kijitonyama Dkt Eliona Kimaro, amewataka vijana kuacha kusubiria vifo kwa kuwa maisha bado yapo na waendelee kuweka mipango yao ya maisha ya kawaida na kuachana na taarifa zinazowaletea msongo wa mawazo.

Mchungaji wa KKKT Kijitonyama Dkt Eliona Kimaro

Hayo ameyabainisha wakati akizungumza na Big Chawa kwenye kipindi cha PlanetBongo ya East Afrika Radio na kueleza kuwa licha ya kuwa janga la Corona limekuwa likiuwa watu wengi katika Mataifa mbalimbali Duniani, lakini vijana wanapaswa kusimama na kulijua kusudi la kuzaliwa kwao.

"Mimi nataka niwaambie watu waachane kabisa na mentality ya kusubiria kufa, hususani vijana, ukishakuwa kijana wa miaka 20-40, umeshaanza kukaa katika mazingira ya kusubiria kifo hiyo siyo sawa, wajue maisha yapo ni muhimu kabisa kuendeleza maisha na wapunguze zile stress za kupata taarifa mbaya, kama idadi ya vifo na wawaze nini kinafuata katika maisha" amesema Mchungaji Kimaro