
"Mfano Maparachichi yakitoka shambani kule Njombe au Tukuyu yaje yafike hapa ni siku ngapi kwamba yakafike yanakoenda si yatakuwa yameharibika! Coldroom iko wapi meneja!", Amehoji Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile na kuagiza kuanza kwa mchakato kujenga chumba hicho.
Meneja wa uwanja wa Ndege Songwe Pascal Kalumbete, amesema uwanja huo umekuwa ukifanikiwa kupata ongezeko la abiria mwaka hadi mwaka na kuishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya uwanja huo ikiwemo kujenga taa za kuingia uwanjani na taa za kuongozea ndege nyakati za usiku ambapo sasa ndege yoyote inawezakutua wakati wowote usiku na mchana.
Kuhusu jengo jipya la abiria amesema baada ya ujenzi huo kutokamilika mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali sasa wamepanga ujenzi huo kukamilika kufikia Desemba 31, 2023 ikiwa sasa umefikia asilimia 98.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Benno Malisa, amesema kukamilika kwa jengo jipya la abiria kutasaidia kuboresha huduma kwa abiria wanaotoka na kwenda katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Malisa amesema pia ujenzi/upanuzi wa Barabara ya njia kutoka Mlimanyoka Uyole hadi uwanjani hapo kutasaidia kuboresha huduma za usafiri na uaafirishaji katika uwanja wa Ndege Songwe