Ijumaa , 1st Mei , 2015

Kuongezeka kwa mtandao wa vituo vya kupima hali ya hewa nchini kunatajwa kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi, ustawi wa jamii na kupambana na majanga kwa ukamilifu zaidi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, (TMA), Dakta Agnes Kijazi.

Katika kuuongezea chachu mpango huo, mkakati unaotajwa kuwepo nchini ni kuandaa programu ya kuhakikisha vituo hivyo vinaimarika na kuwa na vigezo vinavyokubalika na shirika la hali ya hewa duniani (WMO)

Watendaji wakuu kutoka mamlaka ya hali ya hewa na idara ya maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu wamesema kuboreshwa kwa vituo hivyo kutazisaida pia taasisi kupata taarifa zilizo katika viwango vya kimataifa kwa ajili ya shughuli zao zilizokusudiwa

Wakizungumza jijini Arusha na wakuu taasisi zinazomiliki vituo vya hali ya hewa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, (TMA), Dakta Agnes Kijazi pamoja naye mkurugenzi wa idara ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wamesema taasisi hizo zina wajibu wa kuchangia taarifa zao katika “database” ili mamlaka iweze kuzitumia ipasavyo katika shughuli za uchumi kwa ustawi wa jamii..

Akizungumzia mahusiano kati ya Idara ya Maafa na TMA, Brigedia Generali Msuya, amesema ofisi yake imeipatia mamlaka hiyo vifaa vya Shilingi. Bilioni 1.2 kwa ajili ya kusaidia kufanya utabiri wa hali ya hewa..

Taarifa kutoka mamlaka ya hali ya hewa nchini inayoishi kipindi cha robo mwaka inaeleza kwamba maeneo yaliyopo kusini mwa nchi na ziwa Victoria yatapata mvua za juu ya wastani wakati maeneo ya kati, ukanda wa pwani na nyanda za juu Kaskazini mvua zinatarajiwa kuwa chini ya wastani.