Sasa mjadala mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali wa burudani Marekani ni kutaka msanii huyo ashinde tuzo nne tu kati ya vipengele 9 ambapo kwa ushindi wa tuzo hizo atakuwa ameweka historia ya kuwa Rapper mwenye tuzo nyingi zaidi za Grammy duniani.
Kwasasa Rapper anayeshikilia list ya kuwa na tuzo nyingi za Grammy ni Jay Z ambaye ana jumla ya tuzo 25 akifuatiwa na Rapper Kanye West mwenye jumla ya tuzo 24,huku Eminem akiwa na jumla ya tuzo 15, na Pharrell akiwa na tuzo 13.



