Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania, Bi. Jennister Mhagama.
Akizungumza jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya vyuo vya elimu ya juu, Naibu waziri amesema serikali kwa sasa inaanzisha mfumo wa kufundisha masomo ya Sayansi kwa kutumia TEHAMA.
Amesema kumekuwepo kwa dhana kuwa baadhi ya wanafunzi kwamba masomo ya Sayansi ni magumu, hivyo kwa kutumia mfumo wa TEHAMA utasaidia wanafunzi wengi kuvutiwa na masomo hayo.