Dkt. John Rwegasha(kulia) akiwlwza namna ufunguzi wa maonesho ya vifaa tiba ya Medexpo yatakavyosaidi katika kuhamasisha kupambana na upungufu wa vifaa tiba kwenye vituo vya huduma za afya.
Licha ya uwepo wa vituo vya utoaji huduma ya afya baadhi ya wananchi wameeleza kutowepo kwa vifaa tiba vyakutosha na hivyo kulazimika kwenda kwenye maduka ya nje ya hospitali hali inayopelekea wagonjwa kupata huduma kwa haraka.
Queen Simkwassa, Mkazi wa Makumbusho Dar-es-Salaam amesema, "Ukosekanaji wa vifaa tiba Vinakwamisha masuala ya afya mfano unaenda hospitali na kiasi kadhaa unajua unaenda kutibiwa kwa kiasi hiki lakini ukifika pale unaambiwa labda kanunue syringe hapa hakuna".
Ismail Sharif, Mkazi wa Makumbusho Dar-es-Salaam amesema, "Changamoto zipo kwasababu juzi nilikuwa na mgonjwa na kumfikisha hospitali tulihudumiwa lakini baada ya hapo kuna dawa tukaambiwa tukanunue maduka ya nje sasa hali ile sikufurahia maana tunavyokuja hospitali tunatarajia kumaliza kilakitu hospitali".
Ili kupambana na upungufu wa vifaa tiba kwenye vituo vya huduma za afya Daktari Bingwa wa Ini na chakula John Rwegasha katika ufunguzi wa maonesho ya vifaa tiba ya Medexpo ualiyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-es-Salaam ameeleza ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wananchi serikali nikuweka Utaratibu waufikishaji wa vifaa vya kisasa kwa gharama nafuu.
Tumefanikiwa kutembelea mabanda mbalimbali kujionea jinsi ambavyo huduma ya vifaa tiba, madawa yakiwa yametoka matifa mbalimbali kuweza kunyeshwa ni nini kinachoendelea katiaka ulimwengu huu wa tiba ya binadamu.Jitihada ya kufikisha huduma ya vifaa katika ngazi ya chini kabisa kuna taasisi kama MSD ambazo zinasaidia kufikisha huduma hizo mpaka katika zahanati".Dkt. John Rwegasha amesema.
Zaidi mmoja wa wadau wa vifaa tiba amesema kupitia maonesho hayo yatasaidi sekta ya afya katika kupata vifaa vya tiba vya kisasa na kwa bei nafuu.
"Kupitia maonesho haya tumeweza kuwaletea vifaa vya kisasa zaidi ambavyo vitaenda kusaidia jamii na wananchi katika matibabu". Amesema Omary Yasini
Manesho ya vifaa tiba kupitia Medexpo yanalenga katika kuhamasisha upatikanaji wa vifaa vya tiba ilikupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za afya kwa jamii.