Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama
Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP, Tanzania anayeshughulikia miradi Amoni Manyama amesema shirika hilo katika kufanikisha mpango huo linataka kujumuisha zaidi vijana.
Manyama amesema kuwa vijana wanatazamiwa kuongea zaidi katika kuhusishwa kwao katika maendeleo ya nchi kwa wao ndiyo wanaolengwa zaidi katika mpango huo wa maendeleo.
Mkurugenzi huyo amesema ili kufanikisha suala hilo wiki hii kutafanyika kongamano linalowalenga vijana na kwamba wao ndiyo watafaidika zaidi kutokana na kuonekana kuwa ndiyo rasimali ya taifa yenye manufaa zaidi katika ujenzi wa taifa.