
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
Waliosimamishwa ni Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Jamii, Dkt. Nyambura Moremi na Meneja Udhibiti wa ubora Bwana Jacob Lusekelo, ili kupisha uchunguzi wa mwenendo wa Maabara hiyo.
Mbali na kuwasimamisha watumishi hao, Waziri Ummy ameunda kamati ya watalaamu wabobezi ili kuchunguza mwenendo wa maabara hiyo ya taifa ya Jamii.
Kamati hiyo yenye wajumbe 9, inaongozwa na Prof. Eligius Lyamuya, kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili.
Soma taarifa kamili hapo chini