Jumatatu , 8th Aug , 2016

Wafanyabiashara wa nguo aina ya Batiki wanaofanya shughuli zao Machinga Compex Jijini Dar es sa salaam walalamikia ukosefu wa malighafi bora zakutengenezea bidhaa zao na hivyo kuzorotesha ukuaji wa biashara hiyo.

Wafanyabiashara wa Batiki

Wafanyabiashara wa nguo aina ya Batiki wanaofanya shughuli zao Machinga Compex Jijini Dar es sa salaam walalamikia ukosefu wa malighafi bora zakutengenezea bidhaa zao na hivyo kuzorotesha ukuaji wa biashara hiyo.

Wakizungumza na East Africa Television wajasiriamali hao wakiongozwa na bi Rosemery Josephat wameseama malighafi zilizopo kwa sasa hazikidhi viwango vinavyotakiwa na zinauzwa bei ya juu,hali ambayo inapelekea biashara hiyo kudorora.

Nae Grace Mwita na Judith Joel ambao pia ni wajasilimali wa batiki nchini wameiomba serikali kuboresha viwanda vilivyopo kwa sasa ili vizalishe kwa tija ya kwa ushindani.

Kwa upande wake mnunuzi wa bidhaa hizo bi Florah Lyamuya amesema wafanyabiashara hao wawezeshwe kimitaji kwa kupatiwa mikopo yenye riba ndogo.