Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25,oktoba
Wakitoa maoni yao baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza Raisi Mteule wananchi hao wamesema kuwa ni muda wa Watanzania kuacha kufikiria tofauti ya vyama vyao na kufikiria namna ya kuijenga nchi na kuchochea maendeleo ya taifa.
Fredrick Edward mkazi wa jiji la Arusha amesema kuwa kwa sasa wanatarajia mabadiliko makubwa kufuatia ujio wa Rais huyo mpya
Fabian Felician amesema kuwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi watanzania watatakiwa kuhakikisha kuwa wanashirikiana kujenga nchi wa umoja,amani na upendo wakishirikiana na Raisi aliyechaguli bila kujali tofauti za vyama
Mary Lyatuu amesema kuwa anatarajia mabadiliko ya sekta ya elimu ,afya pamoja na miundombinu ambayo yataletwa na Raisi huyo aliyechaguliwa na watanzania wengi.
Haya ni baadhi ya maoni ya wakazi wa Jiji la Arusha juu ya ujio wa Raisi Mpya wa Awamu ya tano John Pombe magufuli huku wakieleza matarajio yao,imani na matumaini waliyonayo kwa kiongozi huyo wa kitaifa .