Ijumaa , 25th Apr , 2014

Wajumbe maalum wa bunge la katiba nchini Tanzania wamesisitiza kurudi bungeni kwa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ili kuweza kujadili kwa pamoja rasimu hiyo ya katiba na kuwapatia wananchi katiba iliyo bora.

Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA), kutoka kushoto Freeman Mbowe wa Chadema, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na James Mbatia wa NCCR Mageuzi, wakiteta jambo katika moja ya vikao vya umoja huo.

Wakichangia katika mjadala wa katiba unaoendelea mjini Dodoma wajumbe hao wamesema kitendo cha wao kususia bunge hilo na kuongea na wananchi ni kuwachanganya wananchi kwa kuwa hoja inayotakiwa kujadiliwa ipo bungeni.

Wamesema kitendo cha UKAWA kuendelea kususia bunge hilo hakitasaidia katika suala zima la upatikanaji wa katiba mpya huku wajumbe wengine wakitaka kuheshimiwa kwa maoni yaliyotolewa na wananchi katika rasimu hiyo ya katiba.