Ijumaa , 17th Mar , 2023

Asasi ya dira ya vijana nchini TYVA imeiomba serikali na wadau wa maendeleo ya vijana kuongeza jitihada za kuhamasisha vijana kushiriki kwenye mchakato wa bajeti kuanzia ngazi ya kijiji. mtaa hadi ngazi ya taifa

Wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu tafiti na uchambuzi mdogo juu ya ushiriki wa vijana kwenye mchakato wa maandalizi ya bajeti viongozi wa asasi hiyo wamependekeza serikali kupitia bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania izingatie vipaombele vya vijana kwenye bajeti ya mwaka 2023/2024 kama vilivyopendekezwa na vijana hao kwenye ripoti ya uchambuzi.

Kwa upande wake meneja ufuatiliaji na tathmini TYVA Hellen Malisa amesema kutokana na ripoti ya uchambuzi wa bajeti kwa jicho la vijana ushiriki wa vijana kwenye bajeti ni mdogo na kinachochangia zaidi ni uelewa ni namna gani Kijana anaweza kushiriki

Akitoa mapendekezo matano kwa serikali mratibu wa miradi TYVA Philipo Mulashani amesema wizara ya fedha na Mipango iondoe tozo na kodi kwenye bidhaa na huduma zinazotoa ajira Kwa vijana wengi hususani za kidigitali na kodi za vifaa vinavyotumika kuzalisha. Kunakili na kusambaza kazi za ubunifu