Fred Felix Minziro amejiunga na timu ya Pamba ya Jijini Mwanza baada ya timu hiyo kumfuta kazi Goran Kopunovic. Pamba imeshacheza michezo saba ya ligi kuu Tanzani bara msimu huu wa 2024-2025 mpaka sasa, imetoka sare michezo minne na kupoteza michezo mitatu na inashikilia mkia katika msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 4.

17 Oct . 2024

Kocha wa zamani wa klabu ya Simba amesaini mkata wa kuitumikia timu ya Al Ahly Tripoli ya nchini Libya. Didie Gomes Da Rosa alikuwa akifundisha timu ya taifa ya Botswana kabla ya kujiuzulu nafasi yake na kutangazwa kwenye klabu hiyo ya Libya kuwa Kocha wao mkuu. Gomes raia wa Ufaransa alishinda taji la ligi kuu Tanzania bara, kombe la shirikisho Tanzania ( FA ) na aliiwezesha klabu ya Wekundu wa Msimbazi kucheza hatua ya robo fainali kombe la klabu bingwa Afrika msimu wa 2021.

17 Oct . 2024

Waziri wa Madini Anthony Mavunde

16 Oct . 2024

Dkt.Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

16 Oct . 2024

Dkt.Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

16 Oct . 2024

Dkt.Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

16 Oct . 2024

Dkt.Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

16 Oct . 2024

Thomas Tuchel kocha wa zamani wa Chelsea ya England amesaini mkataba wa miezi 18 kuiongoza timu ya taifa ya England. Kikosi hicho mabingwa wa kombe la Dunia mwaka 1966 kilikua chini ya Kocha wa muda Lee Carsley baada ya aliyekua Mkufunzi mkuu wa timu hiyo Gareth Southgate kujiuzulu mwezi Julai 2024. Tuchel anakuwa Mwalimu wa tatu ambaye si raia wa Uingereza kuiongoza England baada ya Sven- Goran Eriksson na Fabio Capello. Mjerumani huyo aliyewahi kushinda tuzo ya Kocha bora Ulaya na Dunia mwaka 2021 atasaidiwa na Antony Barry aliyefanya naye kazi Chelsea na Bayern Munich.

16 Oct . 2024

Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United ameujia juu Uongozi wa Manchester United baada ya Mabosi wa klabu hiyo kumuondoa Sir Alex Ferguson kwenye nafasi yake ya Ubalozi wa Mashetani Wekundu wa Jiji la Manchester. Ferguson Kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Mameneja wa Kingereza, aliiongoza Man U kushinda makombe 13 ya ligi kuu Uingereza, Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili na Kombe la klabu bingwa Dunia msimu wa 2007-2008. Cantona alikuwa Mchezaji muhimu alitoa mchango mkubwa kwenye klabu ya Manchester United alishinda makombe ya ligi EPL mara 4 katika miaka 5.

16 Oct . 2024

Picha ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere kulia na Steve Nyerere kushoto

15 Oct . 2024