
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole.
Akizungumza na www.eatv.tv Polepole amesema kuwa mageuzi yatajikita katika maeneo hayo matatu, kwani kila eneo lina vipengele vyake ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya chama.
Polepole amesema kuwa wanaangalia idadi ya watumishi na uwiano wa uzalishaji kama vinaendana, weredi na mahitaji ya rasilimali watu, kiwango cha elimu pamoja na taarifa za wote wanaopokea mshahara kwani amedai kuwa CCM ndio chama pekee chenye watendaji wenye mishahara.
"Tunafanya mageuzi ya CCM, katika nyanja za maendeleo kwakuwa chama ni taasisi, tutafanya mageuzi ya kiuongozi tutaeleza ni viongozi wa namna gani tunaowataka", amesema Polepole.
Polepole amesema kuwa CCM ndio chama kikubwa Afrika, na kina watumishi wilaya zote nchini hivyo, mageuzi hayo yatakuwa na msaada wa kupata taarifa sahihi za uhakiki wa watumishi wake ndani ya chama.
Mageuzi ya Chama hicho kwa wafanyakazi wake, sawa na ule uliofanywa kwa watumishi wa serikali tangu mwaka 2016 ambao uliwabaini zaidi ya watumishi hewa 19,000.
Watumishi hao, walibainika baada ya uhakiki huo kufanyika ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais John Magufuli alilolitoa Machi 15, 2016, ili kubaini uwapo wa watumishi hewa ambao baadhi yao waliendelea kulipwa mishahara licha ya kuwa walikuwa wamefariki dunia, kuacha kazi, kustaafu na kufukuzwa.
Bonyeza link hapo chini, Polepole amefunguka zaidi.