Jumanne , 14th Jun , 2016

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin W. Mkapa amesema kwamba kuna haja ya Watanzania kujiuliza kwa nini katiba mpya ilikwamba na ilikwama kwa namna gani.

Mh. Mkapa ameyasema hayo katika kongamano la kitaaluma lililoandaliwa na kigoda cha Mwl. Nyerere na kufanyika Jijini Dar es salaam ambapo Rais Mstaafu Mkapa ndiye aliyealikwa kama mgeni rasmi.

''Mimi sio mshauri wa Rais, nilitoa maoni kuhusu Katiba Mpya kama nilivyotakiwa hivyo siwezi kulitolea maoni suala hili ila kuna haja ya kufanya uchambuzi''- Amesema Mkapa.

Aidha Mh. Mkapa amewataka watanzania kutambua kwamba nchi hii itaendelezwa na watanzania wenyewe kwani hakuna mtu anayeleta fedha zake kama zawadi bali hileta kuwekeza.

Wakati huo huo Mpaka amewataka watanzania kujikita katika mijadala yenye tija kwa taifa na kuacha kuvipa vipaumbele vitu ambavyo havina mantiki kwa wengi.

Kongamano hilo limejumuisha wanazuoni mbalimbali na kujadili masuala muhimu aliyofanya Rais wa awamu ya kwamza Mwl. Nyerere na masuala yanayoendelea nchini kwa sasa.

Akitoa mchango wake katika kongamano hilo Jenerali Ulimwengu ameitaka serikali kumfikisha mahakamani Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa kusababisha hasara kubwa ya fedha kwa mchakato wa katiba ambayo haikukamilika.