
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye mashine hizo mara baada ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Rais Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mradi wa miundombinu ya utoaji huduma kwa mradi huo wa BRT uliogharimu shilingi bilioni 403 ambapo amesema ujenzi huo utakuwa ni wa jumla ya kilometa 200 ambapo mchakato wa kumpata mkandarasi umeanza na kuwa awamu ya pili itakuwa ni njia ya treni inayoelekea katika mkoa wa Dodoma.
Hata hivyo Rais amewataka mawaziri wa ujenzi, Tamisemi na pamoja na uongozi wa DART kuwasilisha taarifa ya faida ya mradi huo kuanza ili kufahamu kama mradi huo unaendeshwa kwa faida au hasara.
Rais Magufuli akipungia mkono pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop mara baada ya kutoka kukagua comprar viagra moja ya basi linalotumika katika utoaji huduma ya Usafiri wa Haraka (BRT)
"Mawaziri mmetoa taarifa nzuri sana hapa lakini mmeninyima raha kwa kutonipa taarifa ya pesa za faida zilizopatikana kutokana na mradi huu" alisema Rais Magufuli
Amesema alitaka kujua kama zipo fedha za faida za mradi huo ili atoe maagizo kuhusu eneo la Kimara kujengwa kituo kingine kikubwa sehemu ya kuegesha magari ili wenye magari binafsi waegeshe na kupata magari ya mwendo wa haraka.