Jumatatu , 21st Oct , 2024

Naibu waziri wa kilimo David silinde amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kutumia mifumo ya kisasa ya tehama na kuacha kutumia mifumo ya zamani ili waweze kutoa huduma bora katika vyama .

Naibu waziri wa kilimo David silinde amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kutumia mifumo ya kisasa ya tehama na kuacha kutumia mifumo ya zamani ili waweze kutoa huduma bora katika vyama .

Silinde ametoa wito huo  leo October 21 katika  Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ushirika wa akiba na mikopo ya  mwaka 2024 yanayofanyika  jijini mwanza katika uwanja wa mirongo ambapo amesema  matumizi ya tehama niyalazima kama wanataka kuwahudumia  wanachama vyema na kuhimili ushindani uliopo  kwenye soko la fedha waache kujiebdesha kimazowea.

Nae mwenyekiti wa bodi ya chama kikuu cha ushirika wa akiba na mikopo Tanzania SCCULT . Mwl . Aziza Mshana na Benson Diego wamesema wamekuwa wakifanya maadhimisho hayo kwa kila mwaka kwa malengo  kuwakumbuka na kuwaenzi waasisi wa ushirika wa akiba na mikopo kwa mchango wao mkubwa wa kueleza dhana ya akiba na mikopo duniani na Tanzania kwa ujumla .

Maadhimisho haya hayo yanafanyika kwa Siku 5 kuanzia October 20 mwaka huu hadi October 24 mwaka huu yenye kauli mbiu inayosema " ulimwengu mmoja kupitia ushirika wa kifedha " ambayo yana adhimishwa kwa mara ya 76 duniani na kwa mara ya 15 kwa nchini Tanzania tangu kuanzishwa kwake .