Shamba la Kahawa
Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Maendeleo ya Kahawa na uendeshaji wa Bodi ya kahawa nchini, Kajuri Kisenge alipokuwa akizingumza na East Afrika Radio, katika viwanja vya maonesho ya wakulima vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Kisenge, amesema changamoto kubwa inayoikabaili sekta hiyo ni kuporomoka kwa soko la Dunia kunakosababishwa na zao hilo kuzalishwa kwa wingi duniani katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.
Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni tija ndogo katika uzalishaji kutokana na matumizi duni ya pembejeo hususani Mbolea hali inayopelekea kuzalisha kahawa isiyokuwa na ubora unaotakiwa kimataifa.