Pichani ni Harmonize na Pastor Tony Kapola
Sasa msanii Konde ameamua kuwatolea uvivu wadau na mashabiki mbalimbali ambao wametoa mawazo tofauti tofauti kuhusu msanii huyo kuingia kanisani wengine wakihusisha msanii huyo kulipwa na Tony Kapola ili kuonekana kanisani hapo.
"Ukimpa sikio Mungu shetani anawaingia masikioni wanao kuzunguka, so hata ukisema humsikilizi shetani bado utamsikia akiongea kupitia binadamu" Ameandika Harmonize
"Nimekwenda kwa Pastor Tony kutumia muda wangu wa jumapili nione watu wakijifunza,nilitaka kuwa sehemu ambayo Mungu anazungumza, kwa haya yanayoendelea duniani inachekesha kuona baadhi ya watu wakidhani nimelipwa ili mimi kuwa pale" Ameandika Harmonize
''Hakuna mchungaji anaweza nilipa au kununua imani yangu nishavuka huko,najivunia kuwa muislamu,Milele nitaenda kanisani hasa zile zinazofundisha kumjua Mungu na namna ya kuwa mtu mwema na namna ya kutengeneza hela,namna ya kutumia" Ameandika Harmonize