.jpg?itok=DDuM27eD×tamp=1472489916)
Afisa afya wa wilaya ya Same Bw, Aminiel Mnzava amesema licha ya tatizo hilo kuwa kubwa katika maeneo mengi yakiwemo ya Tambarare ni kubwa zaidi katika maeneo ya miinuko na kwamba hata wachache waliojenga vyoo havina ubora na ni tishio kwa usalama wao hasa watoto.
Katibu tawala wa wilaya hiyo Bw. Mashauri Msangi amesema wameanzisha kampeni za kuwahamasisha na kuwawezesha wananchi kujenga vyoo vya gharama nafuu na vinavyotumia maji kidogo zinazofanywa kwa msaada mkubwa wa nchi za Jumuiya ya Ulaya kupitia shirika la Ongawa linalotoa huduma mbalimbali wilayani Same.
Mwakilishi wa shirika hilo la Ongawa Bw, Doda Silivester amesema katika vijiji vilikoanzia kampeni za kuwawezesha wananchi kujenga na kuboresha vyoo mabadiliko yameanza kujitokeza na baadhi ya wananchi wamekiri kuanza kupungua kwa magonjwa.