Jumatatu , 18th Aug , 2014

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka wa bodi ya magavana wa benki BOG utakaofanyika jijini Dar es salaam Agosti 22 mwaka huu.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi nchini Tanzania (kulia) Dkt Servacius Likwelile akiwa na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini Balozi Filberto Sebregondi.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwalile imesema lengo la mkutano huo wa siku moja ni kujadili masuala mbalimbali ya kibank ikiwemo mpango mkakati wa bank hizo na masuala ya fedha na uchumi kwa nchi washirika.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa mkutano huo utatangulia na semina ya wafanyabiashara Agost 21 siku moja kabla ya mkutano mkuu wa magavana.

Wakulima wa pamba jijini Mwanza wameiomba serikali kuwalipa fidia kutokana na kushauriwa kupanda mbegu ya qutoni ambayo karibu misimu mitatu kutotoa mvuno ya kueleweka na kuwatia hasara kutokana na mbegu hiyo.

Wakiongea na naibu waziri wa kilimo, chakula na ushirika Godfrey Zambi jijini Mwanza wakulima hao wamesema kuwa endapo serikali haitawalipa fidia hiyo hali hiyo itawakatisha tamaa kuendelea kulima zao la pamba.

Akijibu hoja hizo naibu waziri amikiri kuwepo kwa changamoto hizo na kusema kuwa serikali ilishasema wakulima wasilazimishwe kulima kilimo cha mkataba na kutumia mbegu hizo lakini pia wameshachukua hatua kwa wakala wa mbegu hizo za quton kwa kutomlipa fedha iliyobakia aliyokuwa anawadai wakulima hao.