Jumatano , 8th Jul , 2015

Serikali imesema kupitia taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imesaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na tatizo la rushwa nchini ikiwemo kuokoa bilioni 12 zilizotaka kuibiwa kwa njia ya rushwa kwa kipindi cha miaka mitano.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma na kuongeza kuwa licha ya viashiria hivyo lakini kuna vigezo vingi vinavyoonesha serikali imeweza kupambana na rushwa ikiwemo ukuaji wa uchumi.

Mh. Mkuchika amesema kwa mujibu wa tafiti za Transparance international inaonyesha kuwa kiwango cha Rushwa nchini Tanzania kinapungua mwaka hadi mwaka na kufanya kuwa ni kati ya nchi zinazopamba na rushwa kwa kiasi kikubwa katika nchi za kusini mwa Afrika.

Aidha Mkuchika ameongeza kuwa kuboreka kwa utoaji wa huduma kwa wananchi ni hatua nyingine inayoonesha kupungua kwa rushwa nchini.

Pia amesema kuwa TAKUKURU imefanya kazi kubwa ikwemo kutoa elimu kwa wananchi juu ya Madhara ya utoaji na upokeaji rushwa elimu ambayo kwa kiasi kikubwa imefanikishwa wananchi kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kutokana kuzijua haki zao.