Alhamisi , 10th Nov , 2016

Taasisi za kifedha nchini bado hazijaonyesha mwamko wa kushiriki uwekezaji kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, kwani mpaka sasa ni benki saba pekee ndizo zimejisajili katika soko hilo

Kauthar D'souza - meneja kutoka The Guardian

Katika soko hilo, kiwango cha biashara kwa sasa kinafikia zaidi ya shilingi za Tanzania trilioni moja kwa mwezi.

Meneja Miradi na Uendelezaji Biashara wa soko hilo Bw. Patrick Mususa amesema hayo leo wakati akizungumzia ushiriki wa DSE kwenye maonyesho ya taasisi za kifedha yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya The Guardian ni mmoja wa wadhamini wa maonesho hayo ambapo meneja anayesimamia alama ya ubora wa magazeti hayo Bi. Kauthar D'souza amesema vyombo vya habari hususani gazeti la The Guardian vina nafasi kubwa ya kukuza ustawi wa sekta ya fedha nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa The Exchange Bw. Aly Ramji amesema wamefanikiwa kutangaza ipasavyo fursa za kiuchumi zilizopo kwenye sekta za madini na fedha nchini, hususani kwa wawekezaji kwenye masoko makubwa ya hisa na fedha kama Marekani, Canada, Uingereza na Mashariki ya Kati.