Dkt. Bashiri Nyangasa Mkurugenzi wa upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Hiyo inatokana na taasisi hiyo kufanikiwa kufanya upasuaji bila kufungua kifua kwa wagonjwa 79 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Dkt. Bashiri Nyangasa ambaye ni Mkurugenzi wa upasuaji wa taasisi hiyo ambapo amesema taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wake wa nje ya nchi wamefanikiwa kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo ambao milango ya moyo ilikuwa haipitishi damu vizuri.
Aidha, Dkt Nyangasa amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia damu kwa hiari kutokana na kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa damu kwa wagonjwa wanaotarajia kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo wameiomba jamii kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara.
