Jumanne , 23rd Nov , 2021

Mtaalam wa masuala ya malezi Singo Mgonja, amesema kwamba vijana wengi wamejijengea fikra za kwamba hakuna ajira kwa kuwa akili zao wameziandaa kwenye suala la kuajiriwa badala ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili ziwapatie kipato.

Mtaalam wa masuala ya malezi Singo Mgonja

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 23, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio.

"Dhana ya kusema hakuna kazi ni mindset, nani anakuambia hakuna kazi, unasemaje hakuna kazi, hilo suala la kusema hakuna ajira ni upumbavu na ujinga, Tanzania kuna fursa ya kila kitu unaweza kufanya chochote na ukafanikiwa," amesema Mgonja.

Aidha, ameongeza kuwa, "Watu wanasema hakuna kazi wakifikiri kazi ni kuajiriwa tu, wanamaliza chuo akili zao ziko kwenye kuajiriwa wakati serikali yenyewe haina wafanyakazi wanaofika laki 5, ukiondoa majeshi na watu wanamaliza karibu laki 2 kila mwaka".