Msanii Shilole.
Akieleza jambo hilo zito kupitia post aliyoweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Shilole ameandika kuwa,
"Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, la kwanza kabisa nataka kuomba radhi kwa jamii yangu kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa haiko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na mengine yasiyozungumzika, naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia pazeni sauti" ameandika Shilole.
"Leo nimeona nivunje ukimya kwamba mume wangu Uchebe amekuwa ananipiga sana, siku 2 zilizopita baada ya kutoka sabasaba kutafutia watoto wangu na kumtafutia yeye nilipigwa sana, sababu za kupigwa ni migogoro ya kawaida ambayo ipo kwenye kila ndoa, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, njia aliyoona ni kunipiga kinyama bila huruma" ameongeza.


