
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya.
Bulaya ameyabainisha hayo leo Mei 6, 2020, wakati wa mazungumzo maalum na kipindi cha Supa Breakfast ya East Afrika Radio na kusema kuwa kama angekuwa ameandika barua basi yeye kama mnadhimu angeipata.
"Kwanza nikanushe Silinde hakuandika barua na kama angeandika mimi kama mnadhimu ningeipata, yeye ni Katibu wa Wabunge na ameupata baada ya kupigiwa kura, sasa Wabunge waliowachagua hawana tena imani nao ni Wabunge ndiyo wamemfurusha kazi kwa usaliti wake, baada ya kuona wabunge wamechachamaa ndiyo kaamua kutumia kivuli cha ku-resign" amesema Ester Bulaya.
Akizungumza na East Afrika Radio, Mbunge Silinde alidai kuwa tayari amekwishamuandikia barua ya kujiuzulu, Mwenyekiti wa chama chake Freeman Mbowe, huku Ester Bulaya naye akikanusha kuwa Silinde hajaandika barua yoyote ile.