Alhamisi , 12th Jun , 2014

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi mpango mkakati wa
kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi hasa kupitia sekta ya kilimo kwa kuanzisha benki ya Kilimo ili kutoa mikopo kwa wakulima kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa mazao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (mahusiano na uratibu) Mhe. Stephen Wassira.

Akiwasilisha taarifa ya Uchumi kwa mwaka wa fedha 2013/2014 na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mhe. Stephen Wassira amesema serikali imejikita zaidi katika mbinu shirikishi za mipango mikakati ya kinga ya jamii hasa kwa makundi ya wanyonge na wasiojiweza.

Wakati huo huo Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Saada Mkuya Salum atawasilisha bajeti ya Trilioni 19.6 katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma muda wowote kuanzia sasa.