Serikali yapiga marufuku hospitali kuzuia maiti

Jumatano , 9th Jun , 2021

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi, ameagiza hospitali zote na vituo vya afya vyote nchini kuacha kushikilia maiti kutokana na deni.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alilolitoa jana katika mkutano wake na Wanawake wa Dodoma.

Akizungumza na wakurugenzi, wakuu wa idara na vitengo wa Wizara ya Afya Prof. Makubi amesema miongozo hiyo imeoanisha makundi maalum ambayo maiti zake zinaachiwa kwa msamaha ikiwa ni pamoja wazee wasiojiweza,watoto wachanga, wanawake wasiojiweza.

Katika hatua nyingine Prof. Makubi amewataka wananchi kuchukua tahadhali za kujikinga na Corona kwa kuwa nchi jirani zimeripotiwa kuwa na wagonjwa, hivyo amewaagiza viongozi kuhakikisha wanahamasisha jamii kuchukua tahadhali kila wakati.