Jumatatu , 11th Jan , 2016

Serikali imewaonya viongozi wa vyama vya akiba vya kuweka na kukopa mkoani Kilimanjaro, kuepuka kuingia katika kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za walala hoi kwa kuwa vitendo vya ubadhirifu ndio chanzo kikuu cha kufa kwa vyama hivyo.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla akikagua kitabu cha utaratibu wa kusajili watalii

Akizungumza mwishoni mwa wiki mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla amesema vitendo kama hivyo vimekuwa vikisababisha vyama kufa hivyo kuwafanya wananchi wengi kukosa imani na vyama hivyo.

Makalla ameongeza kuwa Serikali haitafumbia macho viongozi wote wa vyama vya ushirika ambao watabainika kuhujumu vyama hivyo ambavyo vimeanzishwa na wananchi kwa leo la kujikwamua kiuchumi na kutoka katika lindi la umasikini.