Jumapili , 12th Oct , 2014

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula-NFRA imewatoa hofu wakulima wote waliouza mahindi yao katika msimu huu wa mavuno kuwa watalipwa madai yao yote ndani ya msimu huu.

Naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (kushoto) akiteta jambo la Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Akizungumza jijini Arusha, Afisa Mtendaji mkuu wa NFRA Bw. Charles Walwa amesema kuchelewa kwa malipo hayo kunatokana na kasi ya uagizaji wa mazao ambayo haendani na upatikanaji wa fedha.

Awali katika taarifa yake kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika; Meneja wa NFRA Bw. Bright Mollel amesema hadi kufikiwa Oktoba saba tayari walikuwa wameshavuka lengo la msimu wa manunuzi kwa kununua tani elfu 20 za nafaka.

Hali hiyo inakuja baada ya serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Godfrey Zambi, kuagiza wakala huyo kuhakikisha kuwa mazao yanayonunuliwa ni yale ya kutoka kwa wakulima na sio wafanyabiashara.