
Dkt Ole Nasha ameyasema hyo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Urambo Magreth Sitta aliyetaka kujua ni lini serikali itaondoa tozo za kodi kwenye mbolea ili wakulima waweze kupata mbolea kiurahisi zaidi.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ole Nasha amesema kwamba tatizo la mbolea nchini linatokana na mambo mengi ikiwemo kuagiza mbolea nje ya nchi jambo ambalo linasababisha mbolea kuwa ghali.
Kufuatia hali hiyo tayari serikali ipo kwenye mkakati wa kujenga viwanda vikubwa vya mbolea nchini katika wilaya ya Kilwa na Kibaha.