Alhamisi , 3rd Nov , 2016

Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimeanza mkutano wao hii leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgongano wa kisasa wa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) pamoja na Lesotho.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa

 

Kauli hiyo imetolewa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga, wakati akifungua mkutano wa kamati ya mawaziri wa taasisi ya ulinzi, usalama na siasa ya SADC.

Dkt. Mahiga amesema mgogoro wa kisasa ambao unaendelea kutokea katika nchi hizo ni lazima umalizike mapema ili kuzuia maafa zaidi yasitokee.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa SADC, Stergomena Tax amesema maazimio watakayopitisha na mkutano huo ndiyo utakuwa msimamo wa Jumuiya hiyo ya SADC kwa Congo na Lesotho.