Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko.
Mkutano ambao pia ulihudhuriwa na kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, pamoja na mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) mkoa wa Geita Upendo Peneza mara baada ya zuio hilo viongozi hao waliandika katika kurasa zao za mitandao ya kijamii huku lawama zote wakizielekeza kwa Jeshi la Polisi.
“Jeshi la Polisi linaamuru tuache mkutano wa hadhara hapa Tarime. Mkutano wa kampeni ambao upo kwenye ratiba ya Tume ya Uchaguzi. Msimamizi wa uchaguzi kaamuru mikutano yote ya kata ya Turwa isimamishwe”, ameandika Zitto.
Www.eatv.tv imemtafuta Kamanda wa Polisi Wilayani Tarime Rorya, Henrry Mwaibambe amesema kuwa wanamshikilia Mbunge huyo kwakile alichodai kuwa alikuwa akihamasisha maandamano ya wafuasi wa Chadema.
“Msimamizi wa kituo cha uchaguzi ametuandikia barua akitutaarifu kuzuia kwa mkutano wa hadhara kwa wanachama wa Chadema kwakuwa wamesimamishwa kufanya kampeni kwa muda wa siku nne baada ya kukiuka maadili ya uchaguzi”, amesema Kamanda Mwaibambe.
Msikilize hapo chini Kamanda Mwaibande amefunguka zaidi.